MAHAFALI YA NNE YA KIDATO CHA NNE KATIKA SHULE YA WASICHANA URSULINE

Mnamo tarehe 14/09/2024 shule yetu ilibahatika kufanya mahafali ya nne ya kidato cha nne. Jumla ya wanafunzi 42 walihitimu.

Pichani ni wanafunzi wa kidato cha nne waliofanya mahafali yao 14/09/2024

Mahafali yalianza kwa misa takatifu iliyoongozwa na Mh. Fr. Xavery Mwinuka, paroko msaidizi parokia ya Nyombo.

Baada ya misa lilifuatiwa tukio la kumpokea mgeni rasmi kwa bendi ya shule na kasha kuanza maandamano kuelekea ukumbili. Chini ni video inayoonesha maandamano ya kuelekea ukumbili

Video yenye kuonesha maandamano kuelekea ukumbili tayari kuanza tukio letu la leo

Burudani na maonyesho mbalimbali ya kitaaluma yalitawala ndani ya ukumbi na hivyo kuifanya sherehe ipendeze.

Wimbo wenye kuelezea maana ya moto wa shule yetu
Maandamano kuelekea ukumbini tayari kuanza tukio
Wanafunzi wa kidato cha tatu Ursuline Girls’ wakitupa burudani
Form one wanawaaga dada zao
Dance ya kindi
Waagwa wa kidatom cha nne 2024 Ursuline Girls’
Jaribio la kisayansi

Pia kulikuwa na zoezi la kuwashika walimu mkono kwa kazi kubwa wanayoifanya pamoja na kulishana keki. kiukweli shule yetu inazidi kuongeza juhudi sana katika kuhakikisha taaluma ya inazidi kusonga mbele. hivyo wazazi wameona jitihada kubwa zinazochukuliwa na walimu wetu katika kutokomeza ufaului wa daraja la iv, iii, na hata ii.

tunahitimisha kwa kukiri kuwa sherehe ya kuwaaga wanetu wa kidato cha nne mwaka huu wa 2024 ilipendeza sana.

Waagwa wakitumbuiza

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *